Nchi Iraq vyashambuliwa vituo vya uzalishaji mafuta:
21 Desemba 2003Matangazo
BAGDAD: Nchini Iraq vituo vya uzalishaji wa mafuta vinaendelea kushambuliwa na magaidi. Maafisa wa serikali wamearifu kwamba magaidi wametia moto ghala la akiba ya mafuta katika eneo la mji mkuu Baghdad. Inasemekana moto huo umeteketeza Lita laki kadha za mafuta. Na huko Kusini mwa Baghdad hapo Ijumaa bomba la kusafirishia mafuta liliteketezwa na makombora matatu ya kushambulia vifaru. Mashirika ya habari yaliarifu kuwa polisi wa Iraq wakisaidiwa na wanajeshi wa Kimarekani wamekamata malori 13 yaliyokuwa yakitumiwa katika wizi wa mafuta. Nchini Iraq kuna ubaba mkubwa wa mafuta kwa kuwa kiwango cha uzalishaji wa mafuta kimepunguzwa kwa sababu ya kitisho cha kushambuliwa vituo vya uzalishaji wa mafuta. Kwa sababu hiyo Iraq inalazimika kuagiza mafuta kutoka nchi jirani. Petroli na Diesel hupatikana kwa resheni tu. Tangu aangushwe mtawala wa zamani Saddam Hussein magaidi wamekwisha shambulia zaidi ya vituo 80 vya uzalishaji wa mafuta.