Nchi 4 za Afrika kukosa chakula cha watoto wenye utapiamlo
29 Agosti 2025Matangazo
Shirika hilo lilisema Alhamisi kwamba hali hiyo itachangiwa na uhaba uliosababishwa na kupunguzwa misaada.
Yvonne Arunga, Mkurugenzi wa Save the Children katika eneo la Mashariki na Kusini mwa Afrika, amesema wakati ambapo njaa inazidi kuutikisa ulimwengu, ufadhili ambao unaweza kuokoa maisha ya watoto umepunguzwa kwa sababu ya kukatwa kwa misaada hivi karibuni.
Kwa mujibu wa shirika hilo, ugavi wa vyakula maalum vyenye virutubisho na madini na huduma nyingine za kimatibabu, unapungua zaidi kwenye nchi za Nigeria, Kenya, Somalia na Sudan Kusini.
Baadhi ya zahanati kwenye nchi hizo nne zimegeukia hudumu za matibabu zisizofaa kwa afya ya watoto wenye utapiamlo.