Nato yaahidi kuendelea kuiunga mkono Ukraine
16 Aprili 2025Katibu mkuu wa jumuiya ya kujihami ya NATO, Mark Rutte ameiahidi Ukraine kwamba mfungamano huo wa kijeshi utaendelea kuiunga mkono nchi hiyo dhidi ya mashambulizi ya Urusi. Rutte ameyasema hayo jana wakati akiutembelea mji wa Odessa pamoja na rais Volodymyr Zelensky.Soma pia: NATO yaahidi kuendelea kuiunga mkono Ukraine
Katibu mkuu huyo wa NATO kwenye ujumbe wake aliouandika kwenye mtandao wa X, amesema raia wa Ukraine wamepitia matatizo mengi kutokana na mashambulio ya Urusi ikiwemo shambulio la Jumapili dhidi ya mji wa Sumy, lililosababisha vifo vya tariban watu 35.Soma pia: Mkuu wa NATO asisitiza msaada kwa Ukraine wakati wa ziara Kyiv
Katika mazungumzo na waandishi wa habari, akiwa na Mark Rutte, rais Zelensky alitowa ujumbe kuwatahadharisha wajumbe wa Marekani wanaohusika kwenye mazungumzo na Urusi, dhidi ya kufikia maamuzi yasiyokubalika kuhusiana na maeneo ya Ukraine yanayokamatwa na Urusi.