NATHU LA PASS.India na China zafunguwa tena mpaka wake baada ya miaka 44
6 Julai 2006Matangazo
India na China kwa mara ya kwanza tangu vita vya miaka 44 iliyopita zimefungua mpaka baina ya nchi hizo mbili katika milima ya Himalayas.
Mpaka huo wenye urefu wa mita 4,500 ndio njia pekee ya barabara ya moja kwa moja iliyokuwa ikiziunganisha nchi hizi mbili maarufu.
Maafisa kutoka China na wale kutoka India walivumilia baridi kali na mvua kubwa wakati wa sherehe za kufunguliwa kwa mpaka uliofungwa tangu mwaka 1962.