Nani wakulaumiwa katika mivutano ya ndani Syria?
26 Agosti 2025Zaidi ya mwezi mmoja umepita tangu Hamza al-Amareen atoweke. Raia huyo wa Syria mwenye umri wa miaka 33, ambaye alikuwa mkuu wa kituo cha dharura cha shirika la uokoaji la White Helmets, alitekwa Julai 16 akiwa ndani ya gari lake.
Kabla ya tukio hilo, alikuwa amerudi kutoka kuzima moto maeneo mengine na kusaidia timu ya Umoja wa Mataifa katika zoezi la kuwaokoa watu kufuatia ghasia za hivi karibuni katika jimbo la Sweida, nyumbani kwa jamii ya wachache ya Wadruze.
Ujumbe wa mwisho alioutuma kwa simu ulionyesha kuwa alikuwa akiwasiliana na watu wanaodhaniwa kumteka.Je, njaa inatumika kama silaha ya vita katika maeneo ya migogoro? "Kwa nini atekwe namna hii? Kwa kawaida wafanyakazi wa misaada hawana upande wowote kwenye mapigano,” familia yake iliiambia DW kupitia barua pepe. Wamesema hawana taarifa rasmi kuhusu mahali alipo hadi sasa.
Ripoti za mashirika ya haki za binadamu zinasema kutekwa kwake kunaashiria kuongezeka kwa mvutano wa kijamii kati ya jamii za Wasunni, Wadruze na serikali ya mpito ya kijeshi. Familia yake inahisi huenda Hamza anashikiliwa na wapiganaji wa kidruze kutokana na chimbuko lake la kisunni.
Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni, watu takribani 1,700 wameuawa tangu Julai kutokana na mapigano ya kikabila katika maeneo mbalimbali ya Syria. Mashirika ya haki za binadamu yanasema idadi hii ni sehemu ya ongezeko la vurugu katika mikoa zinakoishi jamii za wachache, ikiwemo ya Alawi.
Wachambuzi wa usalama wanasema SyriaRais wa Syria asema kuunganisha nchi hapaswi kuwa kwa kumwaga damu sasa inakabiliwa na wimbi jipya la machafuko, likijumuisha mauaji ya kulenga watu maalumu, utekaji nyara na ukiukaji wa haki za binadamu. Mzizi wa tatizo hilo, wanasema, ni upungufu wa uthabiti wa serikali ya mpito na mvutano wa makundi ya silaha.
Mapema mwaka huu, serikali ya kijeshi iliahidi kufanya uchunguzi wa kina kufuatia mauaji ya Machi. Ripoti ya uchunguzi iliyotolewa Julai iliwataja watu 298 wanaoshukiwa kuhusika na mauaji, wakiwemo washirika wa karibu wa serikali hiyo ya mpito. Wengine 265 walihusishwa na makundi yanayoiunga mkono serikali iliyopinduliwa ya Bashar al-Assad.
Wiki iliyopita, tume ya Umoja wa Mataifa ilitoa ripoti ya kurasa 66 ikieleza visa vya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, mauaji na utekaji. Ripoti hiyo ilibaini visa 42 na ushahidi wa mashahidi zaidi ya 200,Watu wawili wauawa katika mapigano mapya kusini mwa Syria ikiashiria hali mbaya zaidi kuliko inavyoripotiwa hadharani.
Kwa sasa, familia ya Hamza inaendelea kushinikiza serikali ya mpito kuharakisha juhudi za kumtafuta. Wamesema hawatakoma kupaza sauti hadi wapate jibu au kuona mpendwa wao akiachiliwa huru.