Tangu Agosti mwaka uliopita miili ya watu imekuwa ikiopolewa katika Kingo za Mto Yala huko nchini Kenya. Hadi sasa haijafahamika nani anahusika na mauaji hayo. Tumemkaribisha Alexander Mbela katika Kinagaubaga kutoka shirika la kutetea haki za binadamu Kenya la Haki africa.