MigogoroAfrika
Nangaa: Vikwazo na mkataba wa madini havitamaliza vita Kongo
25 Machi 2025Matangazo
Nangaa anayeongoza muungano huo wa waasi uitwao Congo River Alliance (AFC), ambao unalijumuisha pia kundi la M23 ameyasema hayo alipozungumza na shirika la habari la Associated Press.
Nangaa, amesema watapigana kama watu wasiokuwa na chakupoteza ili kuhakikisha mustakabali bora wa taifa hilo.
Kiongozi huyo wa waasi pia alikataa matokeo ya mkutano wa wiki iliyopita
kati ya viongozi wa Kongo na Rwanda nchini Qatar, na kusema kwamba hatua hiyo ya kutafuta amani bila ya kuhusishwa kwa kundi lake itakosa kufanikiwa .
Nangaa ameongeza kuwa kundi hilo la waasi linaweza tu kufanya mazungumzo na serikali ya Kongo ikiwa nchi hiyo itatambua malalamiko yao na sababu za msingi za mzozo huo.