Teknolojia ya akili mnemba yaani (AI) imeleta mageuzi kwenye nyanja mbalimbali, ikiwemo kwenye sekta ya utawala na uadilifu wa serikali. Kwa kutumia uwezo wake wa kuchambua data kubwa kwa haraka na kwa usahihi, akili mnemba imekuwa nyenzo muhimu kwa serikali katika ufuatiliaji, na kuzuia vitendo vya ufisadi.