SiasaNamibia
Namibia yamwapisha mwanamke wa kwanza kuwa rais
21 Machi 2025Matangazo
Nandi-Ndaitwah mwenye umri wa miaka 72 anakuwa mwanamke wa kwanza kuiongoza Namibia na miongoni mwa wanawake wachache waliowahi kushika wadhifa wa urais kwenye mataifa barani Afrika.
Soma pia: Viongozi mbalimbali waomboleza kifo cha Sam Nujoma
Halfa ya kuapishwa kwake imefanyika ikulu ya nchi hiyo mjini Windhoek na kuhudhuriwa na wakuu wa nchi kadhaa wa Afrika akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania ambaye hadi leo alikuwa ndiye rais pekee mwanamke barani humo.
Nandi-Ndaitwah ambaye hapo kabla alishikilia nafasi ya makamu wa rais, ni kada wa muda mrefu wa chama cha ukombozi wa watu wa Namibia cha SWAPO kilichoiwezesha nchi hiyo kupata huru kutoka Afrika Kusini mwaka 1990.