Nairobi. Polisi wakamata watu waliohusika na mauaji katika kijiji cha Turbi.
19 Julai 2005Matangazo
Polisi nchini Kenya wamewakamata watu saba kwa kuhusika na mauaji ya wiki iliyopita katika kijiji katika eneo la kaskazini , nchini humo huku maelfu ya watu wakiendelea kukimbia nyumba zao wakihofia kulipiziwa kisasi.
Polisi wamesema kuwa miongoni mwa watu hao saba waliotiwa mbaroni, wawili wametambulika kuwa ni viongozi wa mauaji hayo yaliyofanyika siku ya Jumanne katika kijiji cha Turbi ambayo yalisababisha mapambano ya kulipiza kisasi , ambapo jumla ya watu 82 waliuwawa, ikiwa ni pamoja na watoto 26.