Nairobi: Polisi wafyatua mabomu kutawanya wanaharakati
7 Julai 2020Polisi nchini Kenya wamefyatua mabomu ya kutoa machozi na kuwakamata wanaharakati waliojikusanya kwa ajili ya maandamano dhidi ya kile kinachofikiriwa kuwa ni ukosefu wa haki ambao umepewa nguvu mpya mwaka huu kwa madai yaliyotolewa na makundi ya haki za binadamu kuhusiana na ukatili wa polisi wakati wa utekelezaji wa vizuwizi vya ugonjwa wa COVID-19.
Wanaharakati wamesema waandamanaji kutoka maeneo mbali mbali walipanga kufanya maandamano kutoka majumbani mwao hadi katikati ya mji mkuu Nairobi, lakini wengi walitawanywa ama kukamatwa kabla ya kufika katika eneo walilotarajia kukutana.
Samuel Kiiro amesema sita kati ya wenzake kutoka makundi ya haki za binadamu wakfu wa Ghetto katika eneo la mabanda la mathare wamekamatwa.