NAIROBI: Polisi wa kuzima fujo wakabiliana na waandamanaji nchini Kenya
21 Julai 2005Matangazo
Polisi wa kuzima fujo walikabiliana na mamia ya waandamanaji katika barabara za mjini Nairobi Kenya. Wakenya wamekuwa wakiandamana kuyapinga mabadiliko yaliyopendekezwa katika katiba mpya ya taifa hilo, wakisema yanampa rais mamlaka makubwa.
Huku maandamano hayo yakiendelea, baadhi ya waandamanji, wengi wao wakiwa vijana, walivunja maduka na kupora mali na wengine wakavunja magari na kuiba vifaa. Mkuu wa polisi mjini Nairobi amesema mwanamume mmoja alipigwa risasi na kuuwawa kwa kushukiwa kuiba simu za mkononi katika duka moja la simu hizo. Watu kadhaa wamekamatwa na wanahojiwa na polisi.