Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza Angela Rayner ajiuzulu
5 Septemba 2025Matangazo
Kujiuzulu kwa Rayner, mwenye umri wa miaka 45, kunatajwa kuwa pigo kubwa kwa Keir Starmer, kwani ni waziri wa nane na wa ngazi ya juu zaidi kuondoka katika timu yake.
Kuondoka kwake kumeacha pengo la uongozi, hasa ikizingatiwa kuwa Starmer alikuwa amemuunga mkono awali naibu wake huyo wakati shutuma za kodi zilipoibuka.
Wakati chama cha Labour kikipungua kwa umaarufu kwenye kura za maoni, Starmer anakabiliwa na shinikizo la kurejesha mamlaka na taswira ya chama chake.
Rayner alikuwa moja kati ya nguzo muhimu ndani ya chama hicho na kuondoka kwake kunaibua maswali kuhusu uthabiti wa uongozi wa Labour kuelekea uchaguzi mkuu ujao.