Vyombo vya habariUlaya
Naibu mkuu wa zamani wa DW Kiswahili azikwa mjini Cologne
19 Julai 2025Matangazo
Mohammed aliaga dunia Jumanne wiki hii nyumbani kwake Cologne. Alistaafu mwaka 2019 baada ya kuitumikia DW kwa zaidi ya miaka 30 na kutoa mchango mkubwa kwa kizazi cha wanahabari. Miongoni mwa waliohudhuria maziko yake ni watangazaji nguli wastaafu pamoja na wafanyakazi wa DW.
Mohamed Abdulrahman alijiunga na Deutsche Welle mwaka 1980 akitokea nchini Comoro, ambako alikuwa akifanya kazi kwenye shirika la utangazaji la visiwa hivyo vya Bahari ya Hindi, chimbuko la wazee wake.
Waliomfahamu wanamkumbuka kama mwandishi mahiri, mlezi, na mjenzi wa Kiswahili fasaha na sanifu ndani ya DW. Alijulikana si tu kwa sauti yake hewani, bali kwa umahiri wake wa kuandika na kufundisha.