Maslahi ya kimataifa, faida za kiuchumi, mgawanyiko wa kikabila na miungano yenye nguvu vinaunda vita nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ni nani hasa ananufaika wakati waasi wanapochukua miji muhimu na mataifa jirani yakichukua misimamo ya kimkakati? Na kwa nini juhudi za amani kwa miongo kadhaa zimeshindwa?