Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imeanzisha kampeni ya kidiplomasia kupinga biashara ya madini yanayoporwa na Rwanda nchini Congo. Katika mahojiano maalumu na John Kanyunyu wa DW, waziri wa biashara ya nje Julien Paluku alianza kwa kutuambia kwanini wameamua kuanzisha kampeni hiyo sasa na sio zamani kwani, Congo iko kwenye vita yapita miongo tatu sasa.