Mzozo kati ya Israel na Hamas wapamba moto
21 Machi 2025Mashambulizi ya Hamas yanatokea huku Israel ikizidisha pia mashambulizi yake ya ardhini na angani katika Ukanda wa Gaza.
Kwa mujibu wa wizara ya afya inayodhibitiwa na Hamas, mashambulizi ya hivi punde ya Israel, yamewaua Wapalestina 85 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 130, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto.
Soma pia:Amri ya IDF: Wakazi wa Gaza watakiwa tena kuhama
Mbali na mapigano, hali ya kibinaadamu ni mbaya mno huko Gaza ambapo inaarifiwa kuwa bei za bidhaa muhimu zimepanda maradufu. Shirika la habari la Palestina WAFA limesema kuwa kwa sasa kilo moja ya sukari huko Gaza huuzwa dola 10 za Kimarekani.
Hapo jana, kundi la Hamas limeyatolea wito mataifa ya Kiarabu na Kiislamu kuchukua hatua za kukomesha kile ilichotaja kuwa mauaji ya kimbari huko Gaza.