Mwito wa waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani kwa Iran
8 Julai 2006Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank –Walter Steinmeier amewatolea mwito viongozi wa serikali ya Iran wasilikatae pendekezo lililotolewa na mataifa matano yenye kura ya turufu katika baraza la Usalama la Umoja wa mataifa na Ujerumani kuhusu namna ya kuupatia ufumbuzi mzozo uliosababishwa na miradi yake ya kinuklea.Akihojiwa na jarida la Focus,waziri wa mambo ya nchi za nje wa serikali kuu ya Ujerumani amesema ni wajib wa Iran hivi sasa kuamua kati ya kurejea katika meza ya mazungumzo au kujikuta inatengwa kimataifa.Sharti la kumaliza mzozo,anasema waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani ni kwa Iran kuacha kurutubisha maadini ya uranium.Mkuu wa tume ya Iran katika mazungumzo hayo Ali Larijan ameukataa muda uliowekwa na nchi za magharibi kutoa jibu la mapendekezo hayo.