Mwito wa subira wa Kansela Merkel kwa wananchi wa Afghanistan
28 Oktoba 2006Berlin
Kansela Angela Merkel amewasihi wananchi wa Afghanistan wasiingiwe na ghadhabu kufuatia kitendo cha kudhalilishwa wafu kilichofanywa na baadhi ya wanajeshi wa Ujerumani.Katika mahojiano na jarida la Focus,kansela Angela Merkel ametangaza hatua kali dhidi ya wahalifu..Zaidi ya hayo kansela Angela Merkel amesema serikali yake itahakikisha mkisa kama hicho hakitokei tena.Wanajeshi wawili,waliopiga picha wakiwa wanachezea mabufuru ya kichwa na mifupa mengineyo ya binaadam wamesirtishwa kazi.Na watuhumiwa watatu wanaandamwa kisheria.Bwana Peter Struck,ambae kisa hicho kilipojiri alikua waziri wa ulinzi wa serikali kuu ya Ujerumani,amelaani vikali kitendo hicho na kudai hatua kali dhidi ya wahusika.Bwana Peter Struck anasema pachukuliwe hatua itakayokua dawa kwa wanajeshi wote wengine watakaosubutu kufanya visa kama hivyo nchi za nje.