Jeshi lawahoji maafisa wa chama cha Kabila
11 Machi 2025Matangazo
Wito huo unaashiria kile kinachoonekana kama kuongezeka kwa mvutano wa kisiasa kufuatia hatua zilizopigwa na waasi wa M23 mashariki mwa nchi hiyo.
Wakili wa maafisa hao na mshauri wa zamani wa masuala ya usalama wa Kabila Jean Mbuyu amesema sababu hasa ya wito huo bado haikuwa wazi.
Baada ya maafisa hao kutoka kwenye ofisi ya mwendesha mashtaka jana jioni, mmoja wao aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba waliitwa ili kuhojiwa juu ya matamshi yaliyotolewa na Makamu wa rais wa chama hicho Aubin Minaku mnamo Februari 26.
Rais Felix Tshisekedi, aliyewahi kufikia makubaliano tata ya kugawana madaraka na Kabila, amemtuhumu hivi karibuni kwa kuwafadhili waasi wa M23 walioiteka miji miwili mikubwa mashariki mwa Kongo tangu Januari.