Magari ya umeme nchini Kenya yanaanza kuchukua nafasi kubwa katika sekta ya usafiri huku juhudi za serikali na kampuni binafsi zikichochea mabadiliko kuelekea nishati jadidifu. Hata hivyo kuna wasiwasi miongoni mwa madereva kuhusu upatikanaji wa miundombinu ya kuchaji, hasa nje ya miji mikuu. Makala ya Sema Uvume yanaangazia hamasa ya kuendana na mabadiliko ya kidijitali nchini Kenya.