Mwangi na Atuhaire: Tulinyanyaswa kingono Tanzania
3 Juni 2025Matangazo
Wanaharakati wa Kenya na Uganda ambao waliwekwa kizuizini nchini Tanzania wamedai kuwa walinyanyaswa kingono.
Mwangi amesema maafisa wa usalama walimpiga picha huku wakimshambulia. Kwa upande wake Agather Atuhaire amesema na yeye pia alizibwa macho na kushambuliwa kama Mwangi.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters wasemaji wa serikali ya Tanzania, wizara ya mambo ya nje na polisi hawakuweza kupatikana mara moja kujibu tuhuma za wanaharakati hao.
Itakumbukwa, Mwangi na Atuhaire walizuiliwa baada ya kuwasili Dar es Salaam kuhudhuria kesi ya Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania, Tundu Lissu anaekabiliwa na mashtaka ya uhaini.