Utalii wa kupindukia umekuwa tatizo linaloongezeka katika miji mingi na maeneo ya likizo barani Ulaya. Hilo limekuwa changamoto kubwa kwa wakazi wanaolalamika kukosa nafasi zenye utulivu, kupanda kwa bei ya makazi, chakula na bidhaa nyingine muhimu. Baadhi ya nchi sasa zimeanza kuchukua hatua za moja kwa moja kudhibiti mtiririko wa wageni kwa kuweka kodi ya utalii na kuanzisha kikosi maalum.