Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia nchini Austria cha FPÖ kinachoongozwa na Herbert Kickl kimepewa kwa mara ya kwanza katika historia, jukumu la kuongoza mazungumzo ya kuunda serikali baada ya vyama vya jadi kushindwa kuafikiana. Katika hali ya kushangaza, chama cha kihafidhina cha OVP kimekubali kujiunga na FPÖ kwenye mazungumzo hayo.