SiasaUfaransa
Mwanasiasa Le Pen asema anawindwa kisiasa Ufaransa
7 Aprili 2025Matangazo
Le Pen amesema chama chake kinalengwa kwa kuchafuliwa jina. Le Pen amezungumza kwenye mkutano wa hadhara mjini Paris siku sita baada ya mahakama mjini humo kumkuta pamoja na maafisa wengine wa chama cha National Rally - RN na hatia ya ubadhirifu wa fedha za bunge la Ulaya na kuzitumia kwa majukumu ya siasa za ndani.
Le Pen, mwenye umri wa miaka 56, alisema hatokata tamaa. Alipewa kifungo cha miaka minne jela, na miwili ya kifungo cha nje, na akazuiwa kugombea nafasi ya umma kwa miaka mitano. Utafiti wa maoni umemuweka kiongozi huyo wa RN kifua mbele kabla ya uchagizi wa rais miaka miwili ijayo na uamuzi huo wa mahakama umezishangaza siasa za Ufaransa.