Mwanasiasa Kenya auawa kwa kupigwa na risasi mjini Nairobi
1 Mei 2025Polisi nchini Kenya imesema mauaji ya mbunge wa Kenya, Charles Ong'ondo Were, katika mji mkuu Nairobi, yumkini yalikuwa ni ya kupangwa. Mbunge huyo, alipigwa risasi na kuuawa barabarani kwenye mji mkuu wa Nairobi jana Jumatano.
Akilielezea tukio hilo msemaji wa Polisi ya Kenya Muchiri Nyaga amesema kwa namna tukio hilo lilivyotokea inaonekana kwamba uhalifu huo ulipangwa.
Ripoti ya polisi imeeleza kwamba mbunge huyo alipigwa risasi na abiria aliyekuwa kwenye pikipiki wakati yeye akiwa kwenye gari katika Barabara kuu ya Ngong inayokatisha mji mkuu wa Nairobi.
Soma zaidi: Polisi ya Uhispania yawaokoa watoto waliofungiwa kwa miaka 4
Rais William Ruto ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Were na kwa wananchi wa jimbo la Kasipul na kuagiza uchunguzi ufanyike na hatua zichukuliwe kwa waliohusika na shambulio hilo.
Were alikuwa ni mwanachama wa chama cha Orange Democratic Movement, ODM kinachoongozwa na mwanasiasa mkongwe Raila odinga.