Mwanamfalme wa Oslo akabiliwa na mashataka ya ubakaji
28 Juni 2025Mwanamfalme huyo mwenye umri wa miaka 28 anakabiliwa na tuhuma za ubakaji, unyanyasaji wa kingono na kusababisha madhara ya kimwili, baada ya uchunguzi wa miezi kadhaa uliogundua idadi kubwa ya waathiriwa.
Mwendesha mashtaka wa polisi amesema uchunguzi umetegemea ushahidi kutoka kwa mashahidi, ujumbe wa maandishi, na upekuzi wa kina. Licha ya kushirikiana na polisi, Høiby amekanusha mashtaka dhidi yake hasa yanayohusu unyanyasaji wa kingono.
Wakili wake amesema mwanamfalme huyo anachukulia kesi hii kwa uzito mkubwa. Wakati huohuo, Ikulu ya kifalme imetoa taarifa fupi ikithibitisha kuwa mchakato wa kisheria unaendelea kwa mujibu wa taratibu rasmi.
Mwanamfalme Høiby, aliyewahi kufahamika kama "Little Marius,” alikua katika mazingira ya kifalme akifurahia hadhi na neema ya kifalme lakini kwa sasa anaishi peke yake, huku akisubiri hatua zaidi za kisheria akiwa bado anatarajia kutpatikana na hatia wakati mahakama itakapotoa uamuzi.