Mwanajeshi mwengine wa Kimarekani auawa Iraq:
9 Novemba 2003
BAGHDAD: Mwanajeshi mwengine wa Kimarekani ameuawa hii leo liliporipuliwa bomu katika mji mkuu wa Iraq. Jeshi la Marekani liliarifu kuwa alijeruhiwa mwanajeshi wao mwengine katika shambulio hilo lililofanywa barabarani. Hapo Jumamosi usiku mji mkuu Baghdad ulitikiswa na orodha ya mashambulio ya mabomu. Mabomu si chini ya matatu yaliripuliwa baada ya kufanyika orodha ya mashambulio madogo madogo wakati wa mchana. Wanajeshi wa Kimarekani wamekabiliwa na njama za kiasi nchini Iraq, kwa , Richard Armitage. Kule kuendelea kushambuliwa wanajeshi wake kunailetea Marekani matatizo makubwa ya usalama nchini Iraq, alisema Bwana Armitage wakati akiuzuru mji mkuu Baghdad. Wairaq wenyewe wanapaswa kuchukua dhamana zaidi ya kuhakikisha usalama wa ndani, alisema. - Kwa sababu ya kuendelea kitisho hicho cha mashambulio, Chama cha Kimataifa cha Msalaba Mwekundu kimefunga afisi zake katika mji mkuu Baghdad na mjini Basra.