Mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi aachiwa huru
22 Mei 2025Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Musalia Mudavadiamelithibitishia shirika la habari la AFP leo Alhamisi kwamba mwanaharakati maarufu, Boniface Mwangi,ameachiliwa huru na maafisa wa Tanzania.
Mashirika ya haki za binadamu nchi Kenya yamekuwa yakidai kwamba Mwangi alikuwa akizuiliwa mahala kusiko jukulikana,bila ya mawasiliano tangu Jumatatu nchini Tanzania.
Mwangi ni miongoni mwa wanaharakati waliokwenda Dar-es-salaam wiki hii kuonesha mshikamano na kiongozi wa upinzani nchini Tanzania,Tundu Antipass Lissu,wakati alipofikishwa mahakamani kwa mashtaka ya uhaini.
Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty International,limesema Mwangi alikamatwa Jumatatu na kuzuiliwa kusikojulikana na maafisa wa jeshi nchini Tanzania.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Kenya Musalia Mudavadi amesema kuachiliwa kwa Mwangi kumefuatia mazungumzo ya kidiplomasia lakini hakutowa maelezo zaidi.