MWAKA KAMILI KABLA KUANZA KWA KOMBE LA DUNIA UJERUMANI 2006:
9 Juni 2005Argentina kati ya wiki hii iliwachezesha mabingwa wa dunia Brazil katika uwanja wa River Plate, Buenos Aires, kindumbwendumbwe na kuwazaba mabao 3:1. Hivyo, Argentina imekata tiketi yake kwa Kombe lijalo la dunia hapa Ujerumani. Tayari kipindi cha kwanza, Argentina ikiongoza kwa mabao 3:0.
Ilikua kipindi cha pili ndipo Brazil ilipozindukana kutoka usingizi wake kufuatia bao maridadi la mkwaju wa free-kick alilotia Roberto Carlos.Mnamo dakika ya 84 ya mchezo,Adriano, mmoja kati ya washambulizi 4 wa Brazil waliojumuisha Ronaldinho, aligonga mwamba wa lango la Argentina.
Muitikio wa kocha wa Brazil Carlos Parreira kwa pigo hilo ni usemi wake kwamba, pale Brazil ilipoishinda Paraguay mabao 4:1 wiki moja kabla, haikujikuta iko peponi na kwa pigo la jumatano la mabao 3:1 kutoka kwa Argentina haiku motoni.Licha ya pigo hilo,Brazil inahitaji pointi 3 au ushindi mmoja kuifuata Argentina kuja Ujerumani nah ii haina shaka.Kwani, Brazil ndio timu pekee isiopwahi kukosa kucheza finali za kom,be la dunia tangu lilipoanzishwa mjinni Montevideo,Uruguay, 1930.
Kutoka kanda ya Asia,mabingwa wa Asia-Japan ambayo iliandaa Kombe la dunia pamoja na Korea ya Kusini mwaka 2002, imekuwa ya kwanza kutia mfukoni tiketi yake ya kuja Ujerumani.Timu nyengine 3 za kanda hii ambazo zimeshafuzu kushiriki katika Kombe la dunia ni Saudi Arabia,Korea ya Kusini na Iran.Tangu kanda ya Ulaya hata zile za Amerika ya kati na kaskazini na Afrika, bado hakuna timu zilizotia mfukoni tiketi zao za Kombe la dunia-mwaka kamili kabla Juni 9,2006 firimbi kulia kuanzisha Kombe la dunia.
Juni 9,2006 firimbi Italia katika ALLIANZ ARENA mjini Munich, kuanzisha Kombe la dunia.Waziri wa ndani wa Ujerumani ambae wakati huo huo ni waziri wa spoti au michezo siku hiyo atatangaza hivi katika uwanja huo:
“Walimwengu wamekaribishwa nyumbani mwa marafiki zao.
Wageni hawa wastarehe huku kwetu.Hivyo, ndivyo ipasavyo kuwa na hivyo ndivyo itakavyokua.”-asema waziri wa spoti wa Ujerumani bw.Otto Schily.
Kombe la dunia litakua mashindano pekee makuu duniani.Kiasi cha wageni milioni 1 wanatarajiwa kuja Ujerumani kwa Kombe la dunia .Waandazi wa Kombe hilo-Ujerumani-wanatarajia hadi mashabiki milioni 3 kusheheni katika viwanuja mbali mbali vya kombe la dunia.Mashabiki wengine bilioni n30 wanatazamiwa wataangalia Kombe la dunia kwa Tv kutoka kila pembe ya dunia.
Kiuchumi, Ujerumani inatarajia pato lake la kitaifa kuongezeka kwa kima cha 1%.Kuhusu upande huo, mwenyekiti wa Kamati ya maandalio ya Kombe hilo la dunia, Franz Beckenbauer anasema:
“Mtu akiwa na fursa ya muda wa wiki 5 kujitoa hadharani,nafuu ya kujenga jina na heba haihesabiki.”
Kiasi cha Euro bilioni 1.5 zilitumiwa mwaka jana katika kukarabati au kuenga viwanja 12 vitakavyotumika kwa Kombe la dunia.Dimba litachezwa katika viwanja vya miji ifuatayo:Berlin,Munich,Hamburg,Frankfurt-makao makuu ya Shirikisho la dimba la Ujerumani,Cologne,Stuttgart,Dortmund,Gelsenkirchen,Nüremberg,hannover,Kaiserslauten na Leipzig-mashariki mwa Ujerumani.
Tayari viwanja vina nawiri katika hali ya kisasa kabisa vikiwa na zana na mitambo ya video ya kimambo-leo.Katika swali la usalama,wakati wa kombe la dunia hakutakua na mchezo wala uvumilivu kwa wale watakao kuchafua usalama.Wahuni wanaozusha fujo katika viwanja na kandoni mwake wataandamwa barabara sawa na magaidi.Pia kuna kinga tayari za kukabiliana na misiba au misukosuko ikizuka.
Tayari wiki ijayo kati ya Juni 15 hadi 29 Kombe la mashirikisho ya dim,ba-yaani Confederations Cup litatumika kama pazia na majaribio kufungulia Kombe la dunia mwaka mmoja kutoka sasa.Mbali na wenyeji na mabingwa wa dunia mara tatu Ujerumani, watashiriki pia mabingwa wa dunia Brazil,Argentina,Tunesia,Mexico,japan,Australia na Ugiriki-mabingwa wa Ulaya.
Rais wa Shirikisho la kabumbu la Ujerumani (DFB) Theo Zwanziger anaungama:
“Kombe la mashirikisho ni majaribio ya Kombe lijalo la dunia kwavile sisi mjini Frankfurt tunataka kucheza dimba kwa muujibu wa masharti ya Kom be la dunia.Hapa tutafanya majaribio ya uwanjani katika kila upande wa misukosuko inayoweza kutokea.Isitoshe,mtihani tunaokabili kwetu sisi pia ni kama spoti.Kombe hili la dunia ,halitakua na maana ikiwa sisi hatutaunda timu imara itakayoweza kupambana na vishindo vya timu nyengine kali.Na natumai na nataka pawepo hisia barabara uwanjani –hisia za ushabiki wa kombe la dunia.”-asema rais wa Shirikisho la dimba la Ujerumani (DFB) Bw.Zwanziger.
Hata mashabiki wanaona hivyo, kwani tiketi za mechi mbali mbali za Kombe la mashihirikisho-Confederations Cup zimeshauzwa.Pia shauku ya kununua tiketi za kombe la dunia haijapungua.Kwani katika awamu ya kwanza ya kuza tiketi,tiketi laki 8 na 12,000 ziliuzwa.Hivi sasa upepo mpya pia unavuma katika timu ya taifa ya Ujerumani.kocha wa timu hiyo Jürgen Klinsmann tangu kushika wadhifa wake hapo julai 2004 ameelewa baada ya msdiba uliokumba timu hiyo katika Kombe la Ulaya la mataifa nchini Ureno vipi kuihamasisha upya.Na sasa Kombe la shirikisho wiki ijayo ni mtihani kwa timu hii na kwake Klinsmann kujua Ujerumani ni kali namna gain na imejiwinda vipi mwaka kabla Kombe la dunia kuanza.Meneja wa timu ya Taifa ,mshambulizi hatari wa zamani Oliver Bierhoff anasema:
“Kwetu sisi bila shaka ni kombe hili la mashirikisho kujipima nguvu kwavile tutaweza kujua vipi wachezaji wanavyoweza kutamba kwa kipindi kirefu na vipi chini ya shinikizo kubwa la ushindi watacheza katika mechi kadhaa zijazo za kirafiki.”-asema Oliver Bierhoff:
Kwa ufupi Kombe la mashirikisho litadumu wiki mbili kuanzia Juni 15 hadi finali juni 29.Changamoto za kuania tiketi za Kombe la dunia kwa timu 31 kati ya zote 32 itaendelea hadi mwishoni mwa mwaka huu.Ni hapo dezemba 9, baada ya timu hizo zote kutoka kanda mbali mbali kujulikana ndipo kura itapigwa mjini Leipzig kuzigawa katika makundi 8 ya timu 4 -4, kupambana.Rais wa DFB-shirikisho la kabumbu la Ujerumani anamaliza kwa kusema,
“Nadhani pale timu 31 mwishoni mwa mwaka huu zitakapojulikana ndizo zinazokuja kwetu Ujerumani,baada ya kambi zao kutembelewa na kuchaguliwa na tafrija mbali mbali za Kombe hilo kukamilika, ndipo homa hasa ya Kombe la dunia itakapowavaa wajerumani.”-amaliza rais wa Shirikisho la kabumbu la Ujerumani.