Uchumi
Burkina Faso, Mali na Niger kujiondoa rasmi ECOWAS
28 Januari 2025Matangazo
Mnamo Januari 29, 2024, nchi hizo tatu zinazoongozwa na serikali za kijeshi ziliarifu rasmi ECOWAS juu ya uamuzi wa kujiondoa kwao, lakini katiba ya jumuiya hiyo inaeleza kuwa uamuzi kama huo huidhinishwa rasmi baada ya mwaka mmoja.
Burkina Faso, Mali na Niger, ambazo sasa zimeungana katika shirikisho linalofahamika kama Muungano wa Nchi za Sahel (AES), zinaishutumu ECOWAS kwa kuziwekea vikwazo walivyovitaja kuwa vya "kinyama, haramu na visivyo halali" baada ya mapinduzi yaliyowaweka madarakani watawala wa kijeshi.